• elisheshe@yahoo.com
  • +255765837485
  • On: 21 Oct, 2025
  • Admin

Maandalizi ya Kiroho na Kimwili kwa Sadaka ya Ukoo – Vudee 2025

Tunapokaribia Sadaka ya Ukoo – Vudee 2025, tunaitwa kama familia moja ya Mungu kujiandaa kimwili na kiroho kwa shangwe na moyo wa shukrani. Tukiongozwa na Roho Mtakatifu, tutamshukuru Mungu kwa fadhili zake, tutamwomba kwa imani aubariki uzao wetu na kudumisha upendo na umoja kati yetu. Wakati huohuo, tutatafakari Neno lake tukijifunza nguvu ya shukrani na maana ya sadaka impendezayo Mungu. Ni safari ya imani, upendo, na umoja safari ya kumrudishia Mungu utukufu wake. Karibu tujiandae kwa Sadaka ya Ukoo – Vudee 2025

  • On: 21 Oct, 2025
  • Admin

TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUZIDISHA UZAO WETU

Tunamshukuru Mungu kwa kuzidisha uzao wa familia ya Shaidi, kuanzia kwa wazazi wetu hadi vizazi vya wajukuu na vitukuu. Kama uzao wa Ibrahimu kwa imani, tunakumbushwa kuwa baraka na ongezeko vinafuata utii kwa sauti ya Mungu. Tukisikia na kutenda neno lake, tutabarikiwa mjini na mashambani, sisi na uzao wetu wote. Lakini tukikataa, tutaangamia kama asemavyo BWANA. Hivyo, tuombe Roho Mtakatifu atufundishe utii wa kweli, kwani utii ni bora kuliko dhabihu. Tuwe wanyenyekevu na watii, tukimpa Mungu utukufu. Jina la BWANA lihimidiwe. Amen.

  • On: 21 Oct, 2025
  • Admin

TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUULINDA UZAO WETU

Tunamshukuru Mungu kwa ulinzi wake juu ya uzao wetu katika dunia iliyojaa vita vya kimwili na kiroho. Ingawa maadui na nguvu za giza hutuvizia, tuna amani tukijua kuwa vita ni ya BWANA. Yeye ni ngome imara, kimbilio la wenye haki, na mlinzi wa wampendao. Tukimtegemea, kumtii na kulishika neno lake, hatutaogopa maovu, kwa maana gongo na fimbo yake hufariji na kutulinda. Mungu huwahifadhi waadilifu wake na kuwasaidia katika taabu zote. Hivyo, tumtegemee BWANA daima, maana Yeye hulinda uzao wake hata milele. Amen.

  • On: 21 Oct, 2025
  • Admin

Watoto ni Zawadi ya Mungu — Maombi na Shukrani kwa Muumba

Tunamshukuru Mungu Baba wa rehema kwa kutupatia zawadi kuu ya watoto. Kwa unyenyekevu tunawainua mbele zako tukikuomba uwabariki, uwalinde, uwafundishe neno lako, na kuwaongoza katika njia ya kweli wasiiache hata wakiwa wazee. Tunawaweka mikononi mwako ili wakue katika hekima, kimo, na upendo wa Mungu na wanadamu. Wazaliwa wa kwanza tunawainua kwako, kusudi lako litimie juu yao. Wape hekima, maarifa, na nguvu za kutawala na kuongoza. Tunawafunika watoto wetu kwa damu ya Yesu, tukikataa kila mpango wa adui. Utukufu, heshima na sifa ni zako Mungu milele. Amen.

  • On: 21 Oct, 2025
  • Admin

Tunamshukuru Mungu kwa Mafanikio Makubwa Katika Elimu

Tunamshukuru Mungu kwa neema yake kuu aliyoidhihirisha kupitia mzee Shaidi Nziamwe Mkaza, aliyepokea neno la Mungu, kubatizwa mwaka 1914, na kuweka msingi wa elimu katika uzao wake. Ingawa alipingwa na jamii, hakukata tamaa kuwapeleka watoto wote shule, akipanda mbegu ya maarifa inayozidi kuzaa matunda kizazi hadi kizazi. Tunamwomba Mungu aendelee kujaza uzao wetu hekima, akili na maarifa, kama Bezaleli, ili tuwe wabunifu, wavumbuzi, na watumishi wenye heshima kwa Mungu. Elimu yetu iwe chombo cha kumpa utukufu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Amen.

  • On: 21 Oct, 2025
  • Admin

Wosia kwa Ukoo wa Shaidi

Katika mazishi ya Mwl. Marko Shaidi kule Vudee, Baba Askofu (mstaafu) Stephano Msangi alitukumbusha maneno ya Yusufu: “Msigombane njiani,” akitupa wosia wa amani na umoja tusiruhusu mali, chuki au kiburi kututenganisha. Vivyo hivyo, wazazi wetu Mwl. Marko na Mama Merina Shaidi walituusia tuwe na upendo na umoja daima, wakituombea baraka na kutukumbusha maneno ya Zaburi 133:1: “Tazama jinsi ilivyo vyema ndugu wakae pamoja kwa umoja.” Wosia huu wa pacha unatukumbusha kwamba urithi mkuu si mali, bali ni upendo, amani, na umoja unaodumu katika Kristo.

  • On: 21 Oct, 2025
  • Admin

TUMSHUKURU MUNGU WETU

Tunapojiandaa kwa siku ya Marko’s, mioyo yetu ijae shukrani kwa Mungu wetu. Shukrani ni zaidi ya maneno ni ushuhuda wa upendo, imani, na unyenyekevu mbele za Muumba. Ni kumkiri kwa matendo kuwa Yeye ni mwema, rehema zake ni za milele, na neema yake yatutosha. Kama Yesu alivyoshukuru kabla ya muujiza, nasi tushukuru hata kabla ya kuona majibu yetu. Tumshukuru Mungu kwa moyo wote, kwa vinywa vyetu, na kwa matendo yetu, tukimtolea sadaka zetu kama harufu ya manukato ya kumpendeza. Tumshukuru, maana fadhili zake ni za milele.

  • On: 21 Oct, 2025
  • Admin

TUNAKATAA NA KUYAFUTA MANENO YOTE MABAYA YALIYOSEMWA KUHUSU UZAO WETU.

Tunamshukuru Mungu kwa kutulinda na kutuokoa dhidi ya watesi na maneno mabaya yaliyosemwa juu ya uzao wetu. Hata pale ambapo watesi wanazidisha chuki, wivu, na hasira, tunapewa nguvu ya kufuta maneno yote mabaya kwa damu ya Yesu na jina lake. Tukimwamini na kumtii Bwana, tunapata ushindi dhidi ya shetani na uovu wote. Hii ni njia ya kudumu katika imani, shukrani, toba, na rehema, tukijua kuwa Mungu mwaminifu atatusafisha, kutulinda, na kutuwezesha kushuhudia ushindi milele.