Utangulizi Katika Biblia aliyokuwa anaitumia ya United Bible Society, 1952 Mwl. Marko Shaidi kuna maneno ambayo ameyapigia msatari (underline). Mistari iliyopigiwa mstari ni ile ambayo aliiona kuwa ni muhimu kwake na kwetu pia.Nilipitia mistari hiyo tarehe 7 Juni , 2019 na ni rai yangu kuwa tuitafakari mistari hii ili tupate uelewa mpana wa Neno la Mungu. Mistari hiyo ni kama ifuatavyo:-
“BWANA Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya BWANA Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa, na mti wa uzima katikati ya bustani na mti wa ujuzi wa mema na mabaya”.
“Basi akaondoka akaenda Sarepta, hata alipofika langoni pa mji, kumbe! mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni, akamwita, akamwambia, niletee nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa. Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako”.
ZABURI 31:19 “Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako ulizowawekea wakuchao, ulizowatendea wakukimbiliao mbele ya wanadamu”. ZABURI 31:21 “Bwana ahimidiwe, kwa maana amenitendea fadhili za ajabu katika mji wenye boma. ZABURI 32:7 Ndiwe sitara yangu, utanihifadhi na mateso, utanizungusha nyimbo za wokovu.
Utangulizi Wimbo Ulio Bora ni kati ya vitabu vya Biblia vya kishairina cha kipekee zaidi kwa kuwa kinaimba mahaba ya wapenzi wawili mume na mke au bwana na bibi harusi.Pamoja na kusifiana uzuri wa maumbo ya nje yaani maumbile yao , tunaona upendo mkubwa kati yao .Ni jambo jema mume au mke kumsifu mwenza wake lakini zaidi ya yote wapendana na wamsifu kwa pamoja Bwana harusi wetu, Yesu Kristo na tena wampende .
''BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israel asema hivi, mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata’’
“Haya kila aonaye kiu, njoni majini.Naye asiye na maziwa, bila fedha na bila thamani .Kwani kutoa fedha kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii mle kilicho chema, na kujifurahisha nafsi zeni kwa unono.Tegeni masikio yenu , na kunijia , sikieni na nafsi zenu zitaishi, nami nitafanya nanyi agano la milele , Naam rehema za Daudi zilizo imara."
“Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, mwiteni, maadamu yu karibu .Mtu mbaya na aache njia yake na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, naye atamrehemu; na arejee kwa Mungu wetu naye atamsamehe kabisa."
“Maana mtatoka kwa furaha, mtaongozwa kwa amani, mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo, na miti yote ya kondeni itapiga makofi .Badala ya michongoma utamea msonabari, na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili litakuwa la kumpatia BWANA jina, litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali”.
“Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala sio ya mabaya , kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho .Nanyi mtaniita , mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza .Nanyi mtanitafuta na kuniona mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote .Nami nitaonekana kwenu asema BWANA nami nitawarudisha watu wenu waliofungwa, nami nitawakusanya ninyi, nikiwatoa katika mataifa yote na katika mahali pote nilikowafukuza , asema BWANA, nami nitawaleta tena, hata mahali ambapo kutoka hapo naliwafanya mchukuliwe mateka."
“Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku,asubuhi,uaminfu wako ni mkuu. BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, kwa hiyo nitamtumaini yeye. BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, kwa hiyo nafsi imtafutayo. Ni vyema mtu autarajie wokovu wa BWANA na kumngojea kwa utulivu”.
“Nami nitawanyunyizia maji safi, nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa nyinyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, na kuzitenda.Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu”.
“Na walio na hekima watanga’a kama mwangaza wa anga, na hao waongozao wengi kutenda haki watanga’a kama nyota milele na milele.”
“Mnawaza nini juu ya BWANA? Yeye atakomesha kabisa, mateso hayatainuka mara ya pili. Kwa maana wangawa kama miiba iliyotatana, na kunywesha kana kwamba ni katika kunywa kwao, wataliwa kabisa kama mabua makavu”
“Kwa sababu hiyo nawaambieni, msisimbukie maisha yenu,mle nini au mnywe nini, wala miili yenu, mvae nini.Maisha je? Si zaidi ya chakula, mwili zaidi ya mavazi. Waangalieni ndege wa angani ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kuliko hao.”