UTANGULIZI
Kitabu hiki kimeandikwa kwa madhumuni ya kutunza historia ya ukoo wa Shaidi kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo,. Sehemu ya historia hii inatokana na simulizi za mdomo zilizorithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Historia hii isipoandikwa inaweza kutoweka kabisa. Kwa kuwa tupo kwenye enzi za utandawazi hatuna budi kutunza historia hii kwa njia ya maandishi na kielectroniki ili vizazi vyetu viweze kusoma na kuelewa asili na chimbuko la ukoo. Tathmini ya ukoo itawasaidia kutambua hali zipi zinazofanana katika ndugu, hali zipi zimewagusa na kwa kiwango gani na kwa nini hali tofauti tofauti zimezikumba familia katika nyanja za elimu , afya, uchumi na tamaduni. Katika kitabu hiki masuala hayo yote yana angaliwa kwa kuzingatia Neno la Mungu.
Kwa kuwa ukoo wa Shaidi ni mojawapo ya koo za Kipare desturi na mila za Kipare zinaelezwa na jinsi zinavyotekelezwa katika ukoo. Msomaji atagundua kuwa kuna mila na desturi zilizotumika wakati Injili ya Yesu Kristo haijaingia katika Milima ya Upare hasa Vudee na Chome. Ukoo umeshaacha mila na desturi ambazo haziendani na Neno la Mungu. Hata hivyo ukoo unaendelea kudumisha zile ambazo zinampa Mungu sifa na utukufu. Wasomaji wa kitabu hiki wataelewa maisha ya Wapare kabla ya kufika wamisionari na baada ya wamisionari kufika kwa kupitia historia ya ukoo wa Shaidi.
Neno lililotumika katika ukurasa wa kwaza ni kutoka Isaya 60:1 “Ondoka uangaze kwa kuwa nuru yake imekuja na utukufu wa Bwana umekuzukia”. Ukoo wa Shaidi tunatakiwa kuchukua hatua za kuangaza maeneo yote yenye giza katika maisha yetu na ya wengine pia.Giza ni dhambi zetu na Yesu Kristo ndio nuru ya ulimwengu, Zab.27:1 Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu,Nimwogope nani ?Bwana ni ngome ya uzima wangu, nimhofu nani.Katika maisha yetu tunakiri kuwa tumeuona utukufu wa Mungu.
Historia ya ukoo wa Shaidi inaonesha kwa kiasi gani ukoo umepata Baraka nyingi kutoka kwa Mungu.Neno la Mungu linatuonya kwamba “Basi mlapo au mnywapo au mtendapo neno lolote fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu” .Wakorintho 10:31 Kwa kuwa Mungu wetu ndiye anaestahiki kupokea utukufu na heshima na uweza.
Kitabu hiki kinaweza patikana kwa kubofya link hii- BOFYA HAPA