Neno la Mungu linatutaka kufanya maombi na maombezi kwa ajili ya watu wengine, viongozi wa jamii, wasiookolewa, wakristo wenzetu kanisa na wahudumu wake. Katika jambo hili maombi na maombezi yafanyike kulingana na jinsi roho wa Mungu atakavyowaongoza viongozi wa ibada.
Kugundua Ushindi katika Maombi na fifunze jinsi ya kuomba kwa namna inayompendeza Mungu. Kuanzia kuomba kwa jina la Yesu na msaada wa Roho Mtakatifu, hadi kusamehe na kutakasa mioyo yetu. Ingia katika ulimwengu wa maombi yanayokuletea baraka na kujibu kwake."
Kugundua Ushindi katika Maombi na fifunze jinsi ya kuomba kwa namna inayompendeza Mungu. Kuanzia kuomba kwa jina la Yesu na msaada wa Roho Mtakatifu, hadi kusamehe na kutakasa mioyo yetu. Ingia katika ulimwengu wa maombi yanayokuletea baraka na kujibu kwake.
Kugundua Ushindi katika Maombi na fifunze jinsi ya kuomba kwa namna inayompendeza Mungu. Kuanzia kuomba kwa jina la Yesu na msaada wa Roho Mtakatifu, hadi kusamehe na kutakasa mioyo yetu. Ingia katika ulimwengu wa maombi yanayokuletea baraka na kujibu kwake."
SHUKRANI YA PEKEE YA EDNA M.SHAIDI NA VINCENT M.SHAIDI KWA KUFIKISHA UMRI WA MIAKA 70
Maombi ni mawasiliano baina ya binadamu na Mungu au ni njia ambayo tunaweza kuwasiliana na Mungu. Maombi yanaongeza uhusiano wa mtu na Mungu. Maombi ni lazima yafanyike katika jina moja tu lipitalo majina mengine yote Jina lenye nguvu, uweza na mamlaka, Jina la Yesu Kristo (Yohana 14:13-14) Maombi yetu yatakuwa na nguvu ya Mungu iwapo yatafanyika kulingana na mapenzi ya Mungu. Na huu ndio ujasiri tulionao kwake, ya kuwa tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake atasikia (Yohana 5:14) mapenzi yake yanapatikana katika Neno lake Takatifu; “Mapenzi yako yatimizwe hapa Duniani kama yanavyotimizwa huko Mbinguni (Mt6:10).” Maombi yetu yawe sawa sawa na ahadi za Mungu kwetu. Mungu anatualika na kutukaribisha ili tumwombe Mathayo 7:7-8,11 “Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtaona, bisheni nanyi mtafunguliwa. Kwa maana kila aombaye hupokea, naye atafutaye huona, naye abishaye atafunguliwa “Basi ikiwa ninyi mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, Je, Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao? Katika somo letu hili tutatafakari juu ya Nguvu ya Maombi.
Mtu anatoa ushuhuda au taarifa au tangazo la jambo aliloshuhudia au aliloshuhudiwa na mtu mwingine, aliloliona au kulisikia au alilotendewa. Swali kubwa la kujiuliza ni kuwa unashuhudia nini?
Mungu huguswa sana tunaposhukuru kwa moyo wa unyenyekevu, Mungu anatutendea mambo mengi sana lakini tunashindwa kurudisha shukurani ipasavyo. Unatakiwa kurejea mbele za BWANA kwa kushukuru kwa moyo wako wote kama ifuatavyo
Katikati ya utimilifu wa unabii, kukataliwa kwa Yesu kama Masihi aliyetabiriwa na watu wake ni somo kuu la kuchunguza kuhusu kutambua kiroho. Wayahudi, ingawa walipewa utimilifu wa unabii na ishara za ajabu za kuja kwa Kristo, hawakuweza kumtambua. Fundisho hili linachunguza sababu za kutokukubaliana kwao na linachambua tofauti kati ya wale waliomkataa na wale waliompokea kama Mwana wa Mungu na Mwokozi wa ulimwengu.
CHIMBUKO LA SADAKA YA UKOO WA SHAIDI by Neli Msuya Lyaruu
Ukoo wa Shaidi unapatano la kumtolea Mungu sadaka ya shukrani kila baada ya miaka miwili. Sadaka hii inatolewa katika madhabahu ya BWANA katika kijiji cha Vudee au Chome. Tarehe 29/09/2019 wana ukoo walisimama mbele ya madhabahu ya BWANA katika usharika wa Chome na kumtolea BWANA sadaka zao.