TUMSHUKURU MUNGU WETU
Kumshukuru Mungu ni kumuelezea jinsi tunavyomthamini, tunavyomtegemea na kumtamainia, tunavyomheshimu na kumpenda kwa wema wake fadhili zake na baraka zake kwetu.
· Tunamshukuru Mungu aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani ya Bwana wetu Yesu Kristo, ile audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu.
· Siku ya Marko’s day tutamshukuru Mungu kwa vinywa vyetu, mioyo yetu na matendo yetu (Zaburi 9:1-2).
· “Nitamkushuru BWANA kwa moyo wangu wote; nitayasimulia matendo yake yote ya ajabu. Nitafurahi na kukushangilia wewe; nitaliimbia jina lako wewe Uliye juu.
· Tutamshukuru Mungu kwa wema wake na fadhili zake kwetu.
· Zab. 136:/ “mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele”. Wote wa Marko’s na wamchao BWANA na waseme sasa, ya kwamba fadhili zake ni za milele.
· Kumshukuru Mungu ni jambo jema kwa wateule wake Kristo (Wakolosai 3:15). Ni neno jema kumshukuru BWANA, na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu. Kuzingatia rehema zako asubuhi, na uaminifu wako wakati wa usiku (Zab. 92: 1-2).
· Tunatakiwa tudumu katika kumshukuru Mungu bila kukoma (Wakolosai 4:2 na (Wathesalonike 2:13, 5:18). Mungu anatutaka tushukuru kwa kila jambo maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwetu katika Kristo Yesu,
· Tujifunze kushukuru hata kabla ya kupokea kutoka kwa Mungu. Tushukuru kwa imani kwamba jambo tuliloliomba kwa Mungu tayari limetendeka kwenye ulimwengu wa roho na kwamba litatimia kwenye ulimwengu wa mwili.
Tunao mfano mzuri sana wa Bwana wetu Yesu Kristo siku ile alipotwaa ile mikate 5 na samaki 2 alishukuru kabla muujiza ule haujatokea (Marko 6:41).
· Tutakamilisha shukrani zetu kwa Mungu kwa kumtolea sadaka. Tumuombe Mungu azikubali na kuzitakabali sadaka zetu ziwe harufu ya manukato ya kumpendeza.
HITIMISHO
Wapendwa katika Bwana tunapoelekea siku ya Marko’s hatuna budi kufanya maandalizi ya kimwili na kiroho. Ninawaomba kila mmoja wetu aiombee siku hii njema aliyoifanya BWANA machoni petu. Tuendelee kutafakari sifa za ukuu wa Mungu, ili tumwabudu katika roho na kweli. Tutafakari namna nzuri ya kufanya maombi na shukrani. Msifu BWANA kwa matendo yake makuu, mwabudu BWANA kwa uzuri wake. Mshukuru kwa kuwa ni mwema na fadhili zake ni za milele naye atakupa haja za moyo wako. Ninaomba tuhitimishe.kwa kupendekeza “Prayer Items” zetu. Nakuomba uje in-box na pendekezo lako au mapendekezo na mimi nitayaratibu na kuyaweka kwenye group hili. Tumshirikishe Roho Mtakatifu kwa kuwa anajua haja za mioyo yetu. BWANA Mungu atubariki kwa baraka za Haruni (Hesabu 6:24-26) tunapoendelea kumngojea BWANA.