Bwana Yesu asifiwe.Nawaletea siku ya ufunguzi wa Kongamano la wanawake wa Dayosisi ya Pare linaloitwa Askofu na wanawake linalofanyika katika Usharika wa Vudee 12/8/2022 hadi 14/8/2022. Bwana Yesu asifiwe ndugu zangu katika BWANA.Mkutano wa Askofu na wanawake umemalizika juzi Jumapili kwa mafanikio makubwa.Katika kufunga mkutano huo pamoja na mambo mengine Mhe.Baba Askofu ameagiza kuwa majina yote ya mitaa yatumike kulingana na mahali mtaa ulipo.Amesisitiza kuwa hakuna haja ya kupoteza majina yetu na kutumia majina ya Kiisraeli kama vile Sinai, Sayuni, Kana, Bethlehemu, Nazaret, Yerusalem nk; Kwa agizo hilo tunatarajia kupata majina mapya ya mitaa yetu kama wakristo wa eneo husika watakavyoamua.Tupokee maagizo haya kwa mtizamo chana unaompa Mungu utukufu.
Picha na video la tukio hii zinapatikana kwa ku-bofya link hii- BOFYA HAPA.