K.K.T DAYOSISI YA PARE,JIMBO LA MAGHARIBI
RIPOTI YA MABURUDISHO YA WACHUNGAJI
(Na. Mch.Joasi Mpinda)
UTANGULIZI
Maburudisho ya wachungaji na wenzi wao yalikuwa kuwapatia watumishi hawa muda wa kupumzika na kuwaweka mbali kidogo na mazingira ya utumishi wao wa siku kwa siku.Hata hivyo ikapendekeza wasikae tu lakini wapapte muda wa kujifunza jambo jingine litakalowafungua zaidi warejeapo katika vituo vyao.Katika kutafuta kupata jambo la kujifunza katika maburudisho haya ndipo likaja wazo la kujifunza masomo ya Ujasiriamali na Wosia na Mirathi.Kosa kubwa la nchi yetu ni kuondoa somo la Elimu ya kujitegemea mashuleni jambo ambalo limezalisha kizazi tegemezi.Tunamshukuru Mungu kwa ajili ya familia yam zee Vincent Marko Shaidi aliyewekewa utayari wa kugharamikia maburudisho haya kwa asilimia moja Mungu akubariki. ‘’Wapeni watu,nanyi mtapewa kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwa-sukwa hata kumwagika (Luka 6:38)’’
SHUKRANI: Zab 106:1-2,Haleluya Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema,kwa maana Fadhili zake ni za milele.
MAPOKEZI: Mapokezi yalifanyika mnamo tarehe 5/10/2020 saa 11:00 jioni,na mapokezi yalikuwa mazuri.
UFUNGUZI: Ufunguzi ulifanyika tarehe 06/10/2020 saa 3:00 asubuhi ambao ulifanywa na Msaidizi wa Askofu Mch.Timothy Msangi kwa wimbo Namba 310 na neno toka Gal 3:26-29 mkazo ukiwa ni kukombolewa kwa namna ya rohoni kwa njia ya Imani katika Kristo Yesu na tumewekwa huru baada ya ukuta kuondolewa,ukuta wa sheria.
UTAMBULISHO: Tulipata nafasi ya kujitambulisha kwa wenyeji na wenyeji wakajitambulisha kwetu.
SALAAMU MBALIMBALI: Zilitolewa salaamu mbalimbali kama ifuatavyo: ,Msaidizi wa Askofu Mch. Timothy Msangi alitoa salaamu toka Dayosisi ya Mwanga na kwamba alimuwakilisha Mhe. Baba Askofu Chediel Sendoro na mkuu wa jimbo la Tambarare Dayosisi ya Mwanga..Mch Joasi Mpinda Mkuu wa jimbo la Magharibi Dayosisi ya Pare alitoa salaamu za Dayosisi pamoja na salaamu za jimbo. Mhe. Askofu Dr. George M.Fihavango wa Dayosisi ya kusini Njombe alitoa salaamu toka Dayosisi yake,pamoja na wale aliongozana nao ambao ni Katibu mkuu wa Dayosisi Mwl. Grayson C. Shilongoji.
WASHIRIKI
Wachungaji wa Jimbo la Magharibi la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania,Dayosisi ya Pare wakiwa na wenzi wao ambao ni;
1. Mch. Mpinda Joasi na Mwezi wake(Mkuu wa Jimbo)-Vudee.
2. Mch.Mbazieli Kirumbi-Makamu mkuu wa Jimbo -Chome na Suji
3. Mch.Godsoni Nkima na Mwenzi wake-Ngarito.
4. Mch.Joel Mngara na Mwenzi wake-Ivuga.
5. Mch.Elisa Mrutu na Mwenzi wake-Makasa.
6. Mch.Amosi Mrutu na Mwenzi wake-Kirangare.
7. Mch.Eduard Kiseveni na Mwenzi wake-Mwala Papa.
Mch.Elininkanileka Mlemba na Mwenzi wake-Mhero
9. Mch. Emanueli Chediel (Mgane)-Myamba
Mwenzi wa Makamu mkuu wa Jimbo hakuweza kushiriki kwa kuwa walikuwa na msiba wa mwana familia naye alipaswa kubaki nyumbani.
UJASIRIAMALI
Mada hii ilijengwa kwenye kichwa kidogo ,Mchungaji na kumiliki uchumi Asilimia 80% ya maendeleo ya mwanadamu (human development)yanatokana na malezi ya familia.Familia ndiyo inayoanza kumfundisha mtoto kazi (kuosha vyombo),kupika,kufagia,kuomba na kusifu).Lakini huwezi kufundisha ikiwa wewe mwenyewe hufanyi hivyo basi kujitambua ni muhimu sana katika agenda ya kumiliki uchumi. Hata hivyo katika agenda zinazopigwa vita sana kanisani ni hii ya kumiliki uchumi. Maana yake ni nini? Shetani anataka au umiliki uchumi na uache Imani au ukae katika Imani na usimiliki uchumi,lakini kinyume chake ni hakika kwamba unapofanya jambo lolote linalomtukuza Mungu;Mungu atajitukuza kwa namna yoyote (Kumb.8:1-18). Mwanadamu amepewa kumiliki uchumi na kumcha Mungu,’’Amri hii ninayokuamurum leo mtaishika kuitenda mpate kuishi na kuongezeka,’’Ukimtegemea Mungu, yako mafanikio ya wazi (7-10) kwa kuwa BWANA,Mungu wako yuakuingiza katika nchi nzuri yenye vijito na maji na chemichemi,na visima,vibubujikavyo katika mabonde na milima,nchi ya ngano na shayiri na mizabibu na mitini,na mikomamanga,nchi ya mizeituni yenye mafuta na asali,nchi utakayokula mikate humo,pasina shida hutapungukiwa na kitu ndani yake nchi ambayo mawe yake ni chuma ,na milima yake yafukuka shaba.Nawe utakula ushibe, utamshukuru BWANA Mungu wako ,kwa nchi nzuri aliyokupa kumbe hata mahali tunapokanyaga ni chuma, shaba na dhahabu.Hata hivyo kwenye msamiati wa Neno la Mungu hakuna nyumba y a kupanga.(12-14) ‘’Angalia utakapokuwa umekula na kushiba na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake na makundi yako ya ng’ombe na kondoo yatakapoongezeka na fedha yako na dhahabu yako,itakapoongezeka basi hapo moyo wako usiinuke ukamsahau BWANA Mungu wako.Na ukiona kushindwa kwa namna yoyote tambua liko tatizo kubwa la Kimahusiano yako na Mungu.Tafuta njia urudi kwa Mungu.Tnagu uumbaji kusudi la Mungu ni kumilikisha uchumi kwa mwanadamu (mwanzo 1 na 2) baada ya anguko tatizo lilianza ,Ardhi inalaaniwa ,miiba na michongoma inamea na kwa uchungu mwanadamu hujitafutia chakula namna ya kurejeshewa upya wa uumbaji ni kwa kuja Yesu Kristo ka ukombozi wa mtu mzima .Waefeso 1:18-23 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake kwa ajili ya Kanisa ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote. Hata sasa kama hatutembei na Mungu mafanikio ni shida ,Omba kibali cha Mung una ukitembea na kibali cha Mungu hata pale palipokufa panafufuka.Isaya 48:17’’BWANA Mkombozi wako mtakatifu wa Israeli asema hivi,Mimi ni BWANA ,Mungu wako nikufundishaye ili upate faida nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata. ‘’Raha ya kumtegemea Mungu hata kama mwili wa nyama unaumia.lakini mwili wa roho wa ushindi.Inategemea unatazamaje uunapokutana na vikwao,mfano ukirushiwa mawe na kuyaona ni kikwazo yatakuangusha lakini ukiyaona ni fursa unayatumia kujenga daraja.Suala la ujasiriamali ni la kiuwakili na si uwakili wa kutoa tu lakini utapata wapi cha kutoa. Umasikini sio ukosefu wa fedha bali ni kukosa maarifa na uwezo wa kuukataa kwa vitendo. (Hosea 4:6) ‘’Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.Muujiza wa kana ya Galilaya unatafsiriwa kuwa Mungu anajibu maswali yetu katika mazingira yetu.Nikiwa na maarifa ninaweza kuyatambua mazingira yangu.Na kwa kila jambo fanya katika jina la Yesu Kristo (Luka 5:4)Tweka mpaka kilindini.(Yohana 21:6)Litupeni jarife upande wa kuume wa chombo.Sikiliza sauti ya Yesu na usigeuzegeuze.Ni kweli tunafanya kazi na watu waliokata tamaa (Yohana 11:38-44) lakini ni kazi ya kanisa kuwafungua miguu na mikono na kuondoa leso.Tuko katikati ya bonda la mifupa mikavu (Ezakieli 37:1-10) tusiosope bali tuwatabirie watu wabadilike .Mithali 13:22,Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi.Uko msemo unaosema ,kushindwa kupanga ni kapanga kushindwa na kushindwa kujiandaa ni kujiandaa kushindwa.Mchungaji unapostaafu endelea kuwa na sifa ya Mchungaji mwenye ushuhuda na heshima ya kichungaji.
Mhe. Baba Askofu Fihavango, Alikaza kuwa viko vitu vitatu ambavyo tusipoviangalia hutuwezi kushinda umasikini.Alikaza kuwa ujasiriamali ni mgumu lakini umasikini ni mgumu Zaidi.Lakini pia uchumi ni vita ya Kiroho.Pia alionyesha kuwa ujasiriamali usikufanye uache huduma ya kristo.
WOSIA NA MIRATHI
Mada ya pili ambayo ilikuwa kama kichocheo cha kuleta ladha nyingine katika maburudisho haya ilikuwa ya kuwafungua washiriki ufahamu wa kujua jinsi ya kuondoa kabisa mafarakano ya kifamilia na kuacha amani hasa wakati wewe mwenyewe umekufa. Mada hii ilihusu wosia ambapo kwa tafsiri rahisi hii ni kauli inayotolewa na mtu wakati wa uhai wake kwa hiari yake mwenyewe na akiwa na akili yake timamu na mbele ya ushahidi unaoaminika na kukubalika,akionyesha nia yake ya jinsi gani angependa mali yake igawanywe baada ya kufa kwake .Ni tamko la mdomo au la maandishi analolitoa mtu wakati wa uhai wake kueleza jinsi atakavyotaka mwili wake utendewe na mali zake zigawanywe atakapofariki.Wosia sio uchuro kama wengine wanavyoamini.Kisheria tamko hili hutolewa mbele ya mashahidi wanaokubalika na kutiwa sahihi na mhusika mbele ya Ushahidi huo.Aidha wosia huhifadhiwa mahali salama ikiwa ni mahakamani au benki.Mtoa wosia anaweza kubadilisha wosia wake wakati wowote akiwa na akili timamu na mbele ya mashahidi hivyo kuufuta wosia uliotangulia.
FAIDA ZA WOSIA KWA MTOA WOSIA
· Mtoa wosia anapata fursa ya kufanya mgao wa mali zake anavyotaka yeye mwenyewe.
· Mtoa wosia anapata fursa ya kuamua nani awe msimamizi wa mirathi.
· Mtao wosia huepusha magomvi na kuimarisha amani miongoni mwa warithi na ndugu zake.
· Mtoa wosia anayo haki ya kuamua mwili wake utendeweje na mahali gani
· Wosia ni chombo cha kuhakikisha kwamba urithi una kwenda kwa warithi halali.
· Wosia unapunguza gharama na muda wakati wa kuamua mirathi kwa kusoma tu kilichoandikwa.
Mkufunzi wa pili alikuwa Hekaeli Michael Palanjo toka shirika la wanawake wanasheria Tanzania TAWLA,alifundisha juu ya sheria ya ndoa na mirathi, akakaza aina za ndoa,uhalali wa ndoa,haki na wajibu wa wanandoa na Dhana ya ndoa,na alizungumzia juu ya mirathi na kukaza kuwa inaongozwa na sheria tatu ambazo ni za kimila,kiislamu na kiserikali.
Mkufunzi wa tatu ni Mch. Joasi Mpinda Mkuu wa Jimbo.Somo lake lilikuwa ni Maisha ya ndoa. Alitumia neno toka Mh 9:9 na Mathayo 19:3-6 alionyesha mazingira ya uandishi wa Biblia ni ya kimfumo dume. Badala ya kutumia neno mke litumike neno la mwenzi.Pia alionyesha tofauti ya uumaji wa kwanza na wa pili,katika Mwanzo 1:26-27 na Mwanzo 2:14-23.Pia alikaza juu ya maadui watano (5) wa ndoa ambao ni uvivu wa kufanya kazi, tamaa, kukosa uaminifu, upweke na masikio ya punda (kusikiliza maneno ya umbea).
UKARIMU
Tunamshukuru sana ndugu yetu mzee Vincent Shaidi ambaye amejitoa sana kwa unyenyekevu na moyo wake wa upendo na yeye mwenyewe amejitoa kama sadaka kukaa nasi na kutuhudumia mwanzo mpaka mwisho.Huduma tuliyoipokea asubuhi,mchana na jioni na hata wakati wa semina kule ukumbini imetubariki sana. Tunaunganisha shukrani zetu kwa ukarimu huo kwa neno toka Mathayo 10:42.
MALAZI: Tunamshukuru kwa malezi mazuri tuliyoandaliwa ambayo yalikuwa na mahitaji yote.
SALA: Tunamshukuru mkuu wa jimbo la Tambarare Dayosisi ya Mwanga kwa utaratibu aliouweka wa kuongoza sala za asubuhi na jioni zimekuwa Baraka sana.
AZIMIO: Kwa masomo ya Baraka tuliyoyapokea toka kwa wakufunzi wetu,yametupatia elimu ambayo itatusaidia sisi watumishi na familia zetu,pia itawasaidia washirika wetu tunaowahudumia kwa kuwapatia semina na sisi tukiwa vielelezo.
MWISHO: Tunamshukuru Mungu aliyetupa Faragha hii ya maburudisho na semina,tunawashukuru wakufunzi wote,Mkuu wa jimbo la Magharibu la DP na Ofisi yake, Mzee Vincent M. Shaidi pamoja na wahudumu wote walioshughulika kutuandalia chakula.Mungu awabariki sana.