• elisheshe@yahoo.com
  • +255765837485
service photo

Uzinduzi wa Nyumba ya famili ya Marko Shaidi, uliyopo Kijiji cha Vudee, Wilaya ya Same, ni tukio la muhimu kwenye familia.  Nyumba hii inawakilisha jitihada za pamoja kwenye familia kuimarisha mahusiano na kusherehekea historia, tamaduni, na maisha ya familia zetu. Tukio hili ni fursa kwa familia ya Marko Shaidi kuungana pamoja kama familia na kujenga daraja kati ya vizazi vyetu vya sasa na vijavyo. Tunashukuru kila mmoja wenu kwa kushiriki katika kufanya tukio hili kuwa la kipekee na kuhifadhi urithi wa familia ya Marko Shaidi.

Ibada ya ufunguzi iliongozwa na Msaidizi wa Askofu wa dayosi ya Same, Mchungaji Ibrahimu Ndekiya. Neno kuu lilitoka Zaburi 124: 1 " kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi, Israel na aseme sasa". Kwaya iliyohudumu nikutoka usharika wa Mkanyeni

Bofya Hapa kuona video na picha za tukio hili- https://drive.google.com/drive/folders/1CJ_ePqbfs2ikI2u_xxw3VqH1dr7kHzqj?usp=drive_link