• elisheshe@yahoo.com
  • +255765837485
  • 05 Nov, 2023
  • Admin

Marko Mtakatifu 6:38-39

“ Akawaambia , mnayo mikate mingapi? Nendeni mkatazame walipokwisha kujua wakasema , mitano na samaki wawili . Akawaagiza wawaketishe wote, vikao , vikao  penye majani mabichi.”

Katika somo hili  tutatafakari kuhusu maagizo ya Bwana wetu Yesu Kristo kwa wanafunzi wake. Bwana wetu Yesu Kristo katika neno hili alitoa maagizo mawili.Nendeni mkatazame na la pili; Waketisheni wote vikao , vikao,  penye majani mabichi.Wanafunzi wa Bwana Yesu waliwaonea huruma makutano waliomfuata Bwana Yesu kwa kuwa mahali pale hapakuwa na chakula wakamtaka Bwana Yesu awaage waende zao wakajinunulie chakula. Akajibu wapeni ninyi chakula .Wakamwambia, Je! Twende tukanunue   mikate ya dinari mia mbili ili tuwape kula? Akawaambia, mnayo mikate mingapi? Nendeni mkatazame. Hapa tunaona wanafunzi wakitii agizo hilo na kisha kuleta jibu. Je, mimi na wewe Bwana Yesu anatuagiza twende tukatazame nini? Tuanze kwa kutafakari agizo kuhusu. Nendeni na baadaye tutafakari agizo la kutazama. Katika Mathayo 28:19-20 anasema “Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi , mkiwabatiza kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu , na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi, na tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata  ukamilifu wa dahari. Mungu anatuagiza tuwalaishe kondoo wake na kuwatazama wasitawanyike .Yeremia 23:2 “ Kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wa Israeli asema hivi, juu ya wachungaji wanaowalisha watu wangu, mmetawanya kundi langu na kuwafukuza, wala hamkwenda kuwatazama , angalieni, nitawapatiliza uovu wa matendo yenu, asema BWANA”.  Ili tuweze kuifanya kazi hii kwa ukamilifu  ni lazima  tumtazame Bwana wetu Yesu Kristo. Tazama atakuwa pamoja nasi hata ukamilifu wa dahari.Waebrania 12:2” “Tukimtazama Yesu mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu , ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake  aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye  ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu”. Ukiri wa kumtazama Bwana Yesu ulitabiliwa na manabii. Zekaria  12:10 “ Nami nitawamwagia watu  wa nyumba ya Daudi na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba, nao watamtazama yeye ambaye walimchoma, nao wataomboleza kama vile mtu amwombolezeavyo mwanae wa pekee, nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo   uchungu  kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza”.  Naye Yohana Mtakatifu 19:37 anasema kwa maana hayo yalitokea ili andiko litimie; ”na tena andiko lingiine lanena ,watamtazama yeye waliyemchoma.” Jambo hili lilitokea pale msalabani  aliposulubishwa Bwana wetu Yesu Kristo. Yohana 19:34. “Lakini askari mmoja alimchoma ubavu kwa mkuki ;na mara ikatoka damu na maji.”Ufunuo 1:7 “Tanzania yuaja na mawingu ,na kila jicho litamwona ,na hao waliomchoma ;na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake .”Basi na sisi tupige mbio twende tukamtazame Bwana wetu Yesu Kristo tukitafuta kwa bidii kuwa na amani na watu wote ,na huo utakatifu ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao .Waebrania 12:2 “Tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu ;ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu ,naye ameketi mkono wa kiti cha enzi cha Mungu . Pamoja na kumtazama Yesu Kristo Bwana wetu  anatutuma twende kuwatazama wagonjwa ,wajane,yatima,kwa maana hawa ni kondoo wake .Mathayo 25:36. “Nalikuwa uchi , mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni mkanijia”. Bwana Yesu anasema kuwa kadiri mlivyomtendea mmjawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. Wale ambao hawakutenda haki watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele ,bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele. Neno la Mungu katika Yakobo 1:27 linasema “Dini iliyo safi,isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii,kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao,na kujilinda na dunia pasipo mawaa.”Mungu anasema tumtazame  yeye kwanza kwa kuwa hapana Mungu zaidi yake; Mungu mwenye haki ,mwokozi ,hapana mwingine zaidi yake .Isaya 45:22 “Niangalieni mimi, mkaokolewe,enyi ncha zote za dunia;maana mimi ni Mungu; hapana mwingine .”Mbele zake kila goti litapigwa ,na kila ulimi utaapa kwa jina lake. Mungu anayo ahadi njema kwa wale wanaomtumikia  na kumcha  wakati wa mbingu mpya , nchi mpya na Yerusalemu mpya .Ufunuo 21:3-4 “ Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu , naye atafanya maskani yake pamoja nao,  naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwepo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwepo tena, kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita” Tazama atayafanya yote kuwa mapya.  Nakuapia Yesu kukutumikia wewe mfunzi wangu na rafiki mwema .Agizo la pili la Bwana Yesu katika somo hili ni kuwaketisha watu wote vikao vikao,penye majani mabichi. Akatwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili,akatazama mbinguni,akashukuru,akaimega ile mikate akawapa wanafunzi wake wawaandikie ;na wale samaki wawili akawagawia wote, wakala wote wakashiba, na sisi pia tunatumwa twende kwa kondoo wa Bwana tuwalishe  na tutazame na kuona kuwa wameshiba. Mungu anasema sisi ni watu wa malisho yake na kondoo wake.Zaburi 95:6-7 “Njooni,tuabudu,tusujudu, tupige magoti mbele za BWANA liyetuumba. Kwa maana ndiye Mungu wetu, na sisi tu watu wa malisho yake, na kondoo wa mkono wake. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake”. Neno hili Mungu analisisitiza katika Ezekiel 34:31 “ Na ninyi kondoo zangu, kondoo za malisho yangu, ni wanadamu, na mimi ni Mungu wenu, asema Bwana Mungu”. Mungu anasema atawatafuta kondoo zake na kuwalisha yeye mwenyewe atawalisha malisho mema na watalala katika zizi jema.Katika neno hili Mungu anatuonyesha ni kwa jinsi gani tunatakiwa kuwalisha kondoo wake. Bwana wetu Yesu Kristo anataka tuwalishe kondoo wake. Yohana 21:15-21 Bwana wetu Yesu Kristo alimuuliza Simoni Petro swali lile lile mara tatu ; Simoni wa Yohana wanipenda na mara zote akamjibu kuwa nakupenda. Mara ya kwanza Bwana Yesu akamwambia lisha kondoo wangu, mara ya pili akamwambia chunga kondoo wangu na mara ya tatu Yesu akamwambia ,lisha kondoo zangu.Bwana wetu Yesu Kristo anatoa kazi hii kwetu kwa msisitizo mkubwa sana na kututaka tuwachunge kondoo wake  kwa moyo na kuwa vielelezo kwa lile kundi .1 Petro 5:2-4 “Lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu , na  kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo ; si kwa kutaka fedha ya aibu , bali kwa moyo.Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi. Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa , mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyo kauka” Mchungaji mkuu ni Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ametoa uhai wake kwa ajili ya kondoo, huu ni upendo mkuu na wa ajabu sana. Kama unampenda Bwana wetu Yesu Kristo huna budi kuchunga na kulisha kondoo  wake chakula cha uzima.Yohana 6:48-51 , 55-56 “ Mimi ndimi chakula cha uzima. Baba zenu waliila mana jangwani wakafa. Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife.Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni, mtu akila chakula hiki ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni  mwili wangu, kwa ajili ya uzima  wa ulimwengu . Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli , na damu yangu ni kinywaji cha kweli .Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. Hicho ndicho chakula tunachotakiwa kuwalisha kondoo wa Mungu; tuwahubiri juu ya habari njema ya ufalme wa Mungu unaopatikana katika neno lake takatifu. Watu watubu dhambi zao  na kuziacha na kumrudia Mungu. Tuwaketishe watu tuwafundishe habari za Yesu Kristo kwa kuwa twajua hakika kuwa huyu ndiye Mwokozi wa ulimwengu aliyekuja ulimwenguni ili ayatende mapenzi ya Mungu aliyempeleka , akaimalize kazi yake. Mathayo  24:14 Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa Mataifa yote , hapo ndipo ule mwisho utakapokuja”. Tuihubiri habari njema kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyohubiri katika Marko 1 :14-15 .” Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya , akiihubiri, habari njema ya Mungu, akisema wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia , tubuni na kuiamini injili”. Tuihubiri injili ya Yesu Kristo Mwana na Mungu na Bwana wetu kwa utimilifu ambaye katika yeye tulipokea neema na utume ili mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani , kwa ajili ya jina lake. Kusudi mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu, wapate kutii kwa neno na kwa tendo. Usiionee aibu habari njema kwa kuwa ni nguvu za Mungu kwa ajili ya wokovu kwa kila mtu aaminiye .Majani mabichi kwetu ni neema iokoayo ambayo tunapewa bure, neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu. Waefeso 2:8-10 Kwa maana mmeokolewa kwa neema,kwa njia ya imani , ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo  mtu awaye yote asiye akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili twenende nayo”. Neema ya wokovu ya Mungu ni zawadi kutoka kwa Mungu aliyotupa bure kwa sabau ya upendo wake mkuu kwetu. Neema na wema wa Bwana wetu Yesu Kristo vikae nanyi sasa na hata milele.Amina.


·       Akawaambia  mnayo mikate mingapi?

Bwana wetu Yesu Kristo alipowauliza wanafunzi wake mnayo mikate mingapi? Walimjibu mitano na samaki wawili. Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili,akatazama juu mbinguni, akashukuru, akaiibarikia  akaimega ile mikate,akawapa wanafunzi wake wawaandikie;na wale samaki wawili akawagawia wote. Wakala watu wapatao elfu tano wanaume wote wakashiba. Kwa akili za kibinadamu.haiwezekani watu elfu tano wakashiba mikate mitano na samaki wawili zaidi ya hapo wakaokota vipande vilivyomegwa vya kuweza kujaza vikapu kumi na viwili,na vipande vya samaki pia. Katika muujiza huu alioufanya Bwana wetu Yesu Kristo tunajifunza utii kutoka kwa wanafunzi wake kwani walitii kila agizo walilopewa na Bwana wao Yesu Kristo. Tunajifunza pia kuwa kwa BWANA kila kitu kinawezekana ukiwa na imani, utii na tumaini lako kwa BWANA. Marko 10:27 “Yesu akawakazia macho akasema,kwa wanadamu haiwezekani ,bali kwa Mungu sivyo; maana yote yanawezekana kwa Mungu.”Tukiisikia sauti ya Mungu na tukikubali na kutii tutakula mema ya nchi kwa kuwa Mungu atakuwa upande wetu na Mungu akiwapo upande wetu ni nani aliye juu yetu. Kutii ni bora kuliko dhabihu na kusikia kuliko mafuta ya beberu (1 Samweli 15:22). Utii mbele za Mungu ni sifa inayomfanya mtu kupata kibali na baraka za Mungu. Neno la Mungu katika Yeremia 7:23 linasema, “lakini naliwaamuru neno hili, nikisema, sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu; mkaende katika njia ile yote nitakayowaamuru mpate kufanikiwa.” Katika muujiza huu wa Bwana wetu Yesu Kristo na wewe leo hii unaulizwa una mikate mingapi au una kitu gani mkononi mwako ili BWANA akubariki? kila mwenye kitu atapewa na kuongezewa tele lakini asiye na kitu hata kile alicho nacho atanyang’anywa. Kutoka 4; 2-3”BWANA akamwambia (Musa), ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako?Akasema, fimbo. Akamwambia ,itupe chini.” Fimbo ile kuanzia hapo ikawa ni fimbo ya BWANA na siyo ya Musa tena. Mtakumbuka kuwa kwa kutumia ile fimbo ya Mungu, Musa aliweza kufanya ishara nyingi na miujiza. Kutoka 17:8-9 “wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu. Musa akamwambia Yoshua, tuchague watu, ukatoke upigane na   Waameleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile , na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu.” Kwa kutumia fimbo ya Mungu Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga. Katika Wafalme 17:10-16 tunapata mfano mwingine wa Elisha na mama mjane wa Sarepta. Elisha alimwomba mama huyo amletee kipande cha mkate mkononi mwake kwa kuwa Elisha alikuwa na njaa, Naye akasema, “kama BWANA, Mungu wako aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe.” Eliya akamwambia, usiogope, enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee, kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao kwa kuwa BWANA, Mungu wa Israeli,anasema hivi, lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha hata siku ile BWANA atakapoleta  mvua juu ya nchi. Basi akaenda akafanya kama alivyosema Eliya; na yeye mwenyewe, na Eliya na nyumba yake wakala siku nyingi. Lile pipa la unga halikupungua, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa kinywa cha Eliya.” Mama huyu alitii neno la Mungu na akaliamini ndipo akapata muujiza wake wenye baraka tele za Mungu. Ukimtumaini na kumtegemea Mungu yeye hatakupungukia wala kukuacha na kwake hakuna jambo gumu asiloliweza au la kumshinda BWANA. Hata vitu ulivyonavyo vikiwa vichache au dhaifu vya kudharaulika wewe usidharau kidogo ulichonacho kwa kuwa ukimwamini na kumtumaini na kumwangalia Yeye tu atavizidisha na utapata muujiza wako wenye baraka tele. Ayubu 8:7 “Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, lakini mwisho wako ungeongezeka sana. ” Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa, pia; (Luka 16;10). Ukiwa na vichache umtolee Bwana, kwani akiba yako ataiongeza, vipaji vyako haba Yeye hakatai, kidogo kwako wewe kwake kitazidi. Neno la Mungu linatufundisha kuwa hata kama vitu hivyo ni vichache na tena ni dhaifu Mungu anaweza kuvitumia kwa ajili ya kusudi lake na utukufu wake ili jina lake litukuzwe. 1Wakoritho 1:27-28 “Bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima, tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia awaaibishe wenye nguvu,tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya duniani vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko.” Mungu hupenda kuvitumia vyombo vidhaifu kuudhihirisha uweza na nguvu zake ili mwanadamu awaye yote asiye akajisifu mbele za Mungu. Yeye aonaye fahari na aone fahari  juu  ya Bwana. Bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni BWANA.           

 

Share This